Aliyekuwa Seneta wa Trans Nzoia aikosoa serikali kuu kuhusu baa la njaa.

0
163
Aliyekuwa Seneta wa Trans Nzoia Henry Ole Ndiema.

Aliyekuwa Senata wa Kaunti ya Trans-Nzoia Henry Ole Ndiema
ameisuta serikali kuu kwa kile amekitaja kama kukosa kujipanga vyema
katika kushughulikia majanga inayowakumba wananchi kama vile baa la njaa nchini.

Akiongea katika eneo bunge la Endebess Kaunti hiyo Ndiema ameikosoa wizara husika kwa  kukosa kusambaza chakula cha msaada kwa waadhiriwa kwa wakati unaofaa ili hali taifa lina chakula cha kutosha.

Ole Ndiema amegadhabishwa na hatua ya serikali kuzembea kununua mahindi kutoka kwa wakulima kanda ya Northrift  mbali na kujikokota katika  kusambaza pembejeo na mbegu kwa wakulima kwa bei na fuu ilhali ukulima na uzalishaji wa chakula ipo kwenye ajenda kuu nne za
serikali.

Seneta huyo alitilia shaka ufanisi wa miradi hiyo nne kuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here