Mbunge wa Saboti na wenzake watano waisuta serikali kuhusu wakulima.

  0
  271
  Mbunge wa Saboti Caleb Amisi.Picha na Cloud Digital Media.

  Mbunge wa Saboti katika Kaunti ya Trans Nzoia Caleb Amisi,Nandi Hills Alfred Keter na Joshua Kuttuny wa Cheranganyi wamedai kwamba kuna njama ya wafisadi katika Sekta ya kilimo kuagiza mahindi kutoka nje ya nchi ili kujinufaisha jinzi ilivyoshuhudiwa miaka ya hivi majuzi katika sakata ya mahindi ya Mexco.

  Wakiongea katika majengo ya bunge Amisi amesema kwamba wafisadi hao ni wale ambao wamekuwa wakipigia ukulima wa avocado na parachichi upato ili kuwe na njia ya wao kuagiza mahindi kutoka nje.

   Wabunge hao wameitaka Serikali kununua mahindi ya wakulima magunia milioni 25 ambayo bado yako kwa maghala yao kwa bei ya Ksh3, 500.

  Keter alisema kwamba ataakikisha na wenzake kutoka maeneo ya kaskazini mwa bonde la ufa kuzuia wakora wa kuagiza mahindi hawapenyi tena jinzi ilivyofanyika mwaka uliopita ambapo serikali iliagiza mahindi kutoka nje kwa bei ya Ksh 3,900 kwa gunia la kilo 90 ili hali wakulima wakauza mahindi yao kwa bei ya hasara ya Ksh2, 000

  “Agizeni avacado mulishe familia zenu kama munaweza lakini serikali inunue mahindi ya wakulima kwanza kuna mahindi kwa maghala ya wakulima bei ndo ilikuwa mbaya, mbona kuagiza kutoka nje’’ alisema Alfred Keter.

  Serikali kupitia bunge ilikuwa imetenga shilingi billion tano kwa Nafaka ya mazao ya kitaifa kununua mahindi magunia million mbili kutoka kwa wakulima lakini ni magunia 300,000 pekee yaliyonunuliwa baada ya wakulima kulalamikia bei mbovu ya serikali.

   Maeneo ya kaskazini mwa bonde la ufa na maeneo mengine yanayopanda mahindi yalitoa magunia milioni 44 mwaka uliopita.

  Wabunge wengine wanaopigania wakulima ni pamoja na Silas Tiren.

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here