Mwakilishi Wadi ya Machewa apiga shule jeki.

  0
  66
  Wanafunzi wa shule ya chekechea.Picha Maktaba.

  Wanafunzi wa shule ya chekechea katika Wadi ya Machewa eneo bunge la Saboti Kaunti ya Trans-Nzoia wamefaidi zaidi ya madawati 400 kama njia moja wapo ya kuimarisha masomo ya chekechea katika shule za umma kwenye eneo hilo.

  Mwakilishi Wadi ya Machewa Jeff Wambalaba amesema kwa muda mrefu wanafunzi katika shule za chekechea haswa za umma wametelekezwa licha ya kuwa ni msingi wa masomo kwa mwanafunzi, jambo ambalo limepelekea kubuni mbinu mwafaka ya kupiga jeki miundo msingi na vifaa kwa shule hizo.

  Akiongea na Cloud Digital Media Wambalaba amesema ameweka mikakati kuhakikisha wanafunzi wanapata msingi bora wa elimu kupitia kwa ujezi wa madarasa bora kwa shule za chekechea mbali na kupigwa jeki kwa utoaji wa mafunzo ya kiufundi katika vyuo vya anwai katika wadi hiyo.

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here