Mwakilishi Wadi ya Matisi Obed Mwale asababisha tabasamu kwa nyuso za kina mama.

0
354
Baadhi ya Mitungi ya gesi ya kupika iliyotolewa na Mwakilishi Wadi ya Matisi Obed Mwale Mahanga.

Mwakilishi Wadi ya Matisi eneo bunge la Saboti katika Kaunti ya Trans Nzoia Obedi Mwale Mahanga (ANC) amewashangaza wengi hasa wenyeji baada ya kutimiza ahadi aliyoitoa wakati wa Kampeni za uchaguzi wa 2017.

Maelefu ya kina Mama walipewa mitungi ya gesi ya kupika katika oparesheni ‘ondoa moshi jikoni’ ambayo wandani wake walisema itaendelea.

Katika hotuba yake na Cloud Digital News,Obed alisema kwamba atafanya chochote atakachoweza ili kuboresha maisha ya waliomchagua ikiwemo usambasaji maji,barabara,kuweka taa za usalama na maendeleo mengine.

‘’Nimeishi hii Trans Nzoia tangu nizaliwe mwaka wa 1962 na sijawai kuona mwanasiasa kama huyu ambaye ashafanya hivo kwa wapiga kura wamama wamefurahi na hii oparesheni ya kuondoa moshi jikoni’’ alisema Alice Nakhumicha.

Mwakilishi Wadi ya Matisi Obed Mwale Mahanga(kulia- mwenye suti) akionyesha baadhi ya mtungi wa gesi kwenye hotuba yake.

Aidha wananchi walimpongeza Obed kwa uongozi wake ikiwa ni muhula wake wa kwanza wakiwataka viongozi wengine wa Wadi mbalimbali kufanya vitu vinavyoenekana.

Wadi ya Matisi ina wapiga kura 22,738 kulingana na data ya Tume ya Uchaguzi (IEBC) ya 2017.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here