TIMU YA SOKA YA BATOTO BA MUNGU ELIM YATESA.

  0
  166
  Picha:Kikosi cha Elim Youths Wakiwa na Tim Oduor

  Mbali na kulishwa chakula cha kiroho vijana pia vipaji vyao vinapaliliwa kupitia soka na watumishi wa Mungu wa kanisa la Elim Kitale uwanjani ambao wamejitolea kuwalea vijana kutoka jamii mbali mbali kaunti ya Trans-Nzoia.

  Ninayo izungumzia sio nyingine mbali ni timu ya Soka ya Elim Youth FC ambayo ilibuniwa miaka mitatu iliyopita kwa minajili ya kuendeleza vipaji vya vijana. Na kwa sasa vijana wa Elim Youth wamekuwa kero kwa timu zingine licha ya kubuniwa hivi majuzi tu inatesa vigogo wa zamani uwanjani na kuwa kizingiti ki kuu kwa wapinzani wao ugenini na nyumbani.

  Elim Youth FC chini ya kanisa la Elim lenye makao makuu Village inn kwenye barabara kuu kutoka Kitale -Eldoret chini ya mlezi Askofu Simon Githigi,timu maneja Boniface Odour Wod Nyonga kod Joseph jinsi TM huyo anavyo julikana,mwenyekiti Kasisi Laban Macharia,katibu Kasisi Patrick Mulei naye mkufunzi mkuu ni Peter Imo.

  Viongozi hawa waliona ni vyema kukuza na kupalilia vipaji vya vijana vya kiroho na vya michezo wakaita vijana na kuwaweka pamoja na kuanzisha timu,timu hii ya Elim Youth kabla ianzishwa miaka mitatu iliyopita kulikuwa na timu ya vijana wasiozidi miaka 13-15 kwa zaidi
  ya miaka 12 ndipo kamati ikamua kuanzisha ya vijana wa kuanzia miaka 16-25.

  Akiongea na Taifaleo makala ya spoti Askofu Githigi alisema waliona njia kuu ya kuwaleta vijana kwa kristo na kutumia michezo ili vijana wasiingie kwa mambo ya kutumia madawa ya kulevya baada ya kumaliza shule. Alsema kuwa pia waliona vijana ni mabalozi wema wa kuleta utengamano kwa jamii na kukuza amani ambayo ndio msingi wa maendeleo.


  “Kuna njia nyingi za kuleta vijana pamoja na wengi hutumia njia za kuandaa krusedi,kwaya na mahubiri kupitia nyimbo,lakini sisi tuliamua kutumia michezo kuwavutia vijana ili kuwaleta kwa Mungu na tumefaulu kuwaleta vijana wengi sana na wamebandilika na kuanza kumtumikia Mungu”akasema Askofu Githigi.

  Timu maneja Odour naye alisema vijana wengi wamekuwa wakipoteza imani baada ya kumaliza shule na kukosa ajira,alisema hilo pia ni jambo ambalo liliwapa changamoto na kuamua kuanzisha timu ili kukuza vipaji vya vijana. Alisema michezo hulipa na kumuweka kijana kwa maisha mazuri ikiwa ataweza kupata klabu cha kuchezea.

  Timu hii sasa inashiriki kwenye ligi ya FKF daraja la pili kanda ‘B’ na iko kwenye nafasi nzuri hivi majuzi iweza kusafiri hadi Lodwar Kaunti ya Turkana mechi ya kwanza walisakata na Nawaitarong fc ya Ladwar na kutoka 1-1,uga wa Lodwar mechi ya pili walicheza na Kakuma
  wakafungwa 2-1,wakarudi nyumbani na kucheza na vijana wa Chewoyet kutoka Pokot na kuwalima Chewoyet 3-1,walisafiri hadi Eldoret kucheza na Blitz,Elim ikatoshana kwa kufungana 1-1 uga wa Pipeline mjini Eldoret.

  Odour alisema Kaunti ya Trans-Nzoia licha ya kujulikana ka kapu ya Kenya kwa kukuza Mahindi alitaja pia ukuzaji au uzalishaji wa vijana waume kwa wake ambao wana talanta ya kusakata soka na kufika mbali. Alisema timu hii inajivunia wachezaji wahitaji ka vile kipa David Simiyu, Douglas Okumu (6),Moses Maina (9/11),Dennis Opiyo (10),Alphonce Arondo (5),Solomon Matoni (8),Stephen Kusinjilu (2) na Isaya Ocheni (3).

  Katibu wa timu Mulei ambaye pia ni kasisi alitoa wito kwa wazazi wasiwazuie wanao kushiriki mchezo wa soka,akisema kuwa huenda ni mahali ambapo Mungu amemuwekea huyo mtoto bahati yake ya ajira. Alisema hivi karibu wataanzisha akademi ya kukuza talanta za soka kwa vijana wa kike na wa kiume wa miaka 12 wakifika miaka 15 wanaingia kwa timu ya under 16 na kuendelea.

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here